Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 30, 2018, limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7.22 ikilinganisha na mwaka 2016.
Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Charles Msonde ameeleza kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 7.22 huku watahiniwa 265 wakifutiwa matokeo kwa udanganyifu wakiwemo wanafunzi 136 waliofanya mtihani wa kujitegemea (Private Candidate) na 129 waliofanya mtihani wa shule (School Candidate).
Amemtaja mwanafunzi aliyeongoza kitaifa kuwa ni Ferson Mdee kutoka Shule ya Sekondari Marian Boys.
0 Comments